Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Mashhad, Hujjatul-Islam Sheikh Muin Daqiq, mwakilishi wa Hizbullah ya Lebanon nchini Iran, Jumanne tarehe 12 Khordad (2 June 2026), katika Kongamano la Pili la Kimataifa la Ghadir na Muqawama linalofanyika katika eneo la Imamzade Yahya bin Zayd mjini Miyami, Mashhad, alisoma ujumbe wa Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon.
Matini ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:
Kongamano la Pili la Ghadir na Muqawama
Idi ya Ghadir: Dira ya Uongofu
Waheshimiwa wanazuoni, walimu na washiriki wa Kongamano la Ghadir na Muqawama, Mwenyezi Mungu awatukuze.
السلام علیکم ورحمة الله وبرکاته
Mwenyezi Mungu ametuneemesha kwa kutupa Uislamu na kumtuma Mtume Wake Muhammad (saww) kuwa mwongozo, mtoaji wa bishara njema na mwonyaji kwetu, aliweka wazi njia ya uongofu wa Umma na mwendelezo wake kupitia Wilayah ya Bwana wa Mawasii, Imam Ali (as), ili mnyororo wa imani ujengwe juu ya ardhi; mnyororo ambao umeunganishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na unaanzia kwa Mtume hadi kwa Imam na mfululizo wa Maimamu (as), kisha unaendelea katika mkusanyiko mkubwa wa kibinadamu duniani ambao unajulikana kwa jina la Hizbullah.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:
{إِنَّمَا وَلِیُّکُمُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِینَ آمَنُوا الَّذِینَ یُقِیمُونَ الصَّلَاةَ وَیُؤْتُونَ الزَّکَاةَ وَهُمْ رَاکِعُونَ}
"Hakika kiongozi na mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na kutoa Zaka hali ya kuwa wako katika rukuu."
{وَمَنْ یَتَوَلَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَالَّذِینَ آمَنُوا فَإِنَّ حِزْبَ اللَّهِ هُمُ الْغَالِبُونَ}
(Surat Al-Ma'idah: 55–56)"Na atakaye fanya urafiki na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, basi hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kushinda.."
Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema:
مَنْ سَرَّهُ أَنْ یَحْیَا حَیَاتِی وَیَمُوتَ مَمَاتِی، وَیَسْکُنَ جَنَّةَ عَدْنٍ غَرَسَهَا رَبِّی، فَلْیُوَالِ عَلِیًّا مِنْ بَعْدِی، وَلْیُوَالِ وَلِیَّهُ، وَلْیَقْتَدِ بِأَهْلِ بَیْتِی مِنْ بَعْدِی، فَإِنَّهُمْ عِتْرَتِی، خُلِقُوا مِنْ طِینَتِی، وَرُزِقُوا فَهْمِی وَعِلْمِی، فَوَیْلٌ لِلْمُکَذِّبِینَ بِفَضْلِهِمْ مِنْ أُمَّتِی الْقَاطِعِینَ فِیهِمْ صِلَتِی، لَا أَنَالَهُمُ اللَّهُ شَفَاعَتِی
"Yeyote anayefurahia kuishi maisha kama yangu, kufa kifo kama changu na kuishi katika Pepo ya Adn aliyoiotesha Mola wangu, basi ampende Ali baada yangu, awapende marafiki wake, na afuate Ahlul-Bayt wangu baada yangu. Hakika wao ni kizazi changu, wameumbwa kutokana na asili yangu, na wamepewa ufahamu na elimu yangu. Ole wao wale wanaokanusha fadhila zao katika Umma wangu na wanaokata uhusiano wangu nao; Mwenyezi Mungu asiwafikishie uombezi wangu."
Idi ya Ghadir ni mkamilishaji wa hoja, mthibitishaji wa njia ya haki, mwenye kuimarisha matumaini, na dira ya uongofu pamoja na chemchemi ya kheri na wema.
Idi hii iwe ya baraka kwenu — Kila mwaka muwe katika heri.
Hizbullah ya Lebanon ilianzishwa baada ya uvamizi wa Israel ambao ulifika hadi mji mkuu wa Beirut mwaka 1982, kupitia kiapo cha utii cha kundi la Waumini kwa Kiongozi wa Mapinduzi, Umma na Walii wa mambo ya Waislamu, Imam Khomeini (qds). Yeye alikubali kiapo hicho na akatuongoza kuelekea kipaumbele cha kuisaidia Palestina na kukabiliana na adui Muisraeli kwa msingi wa imani na vitendo ndani ya mfumo wa umoja wa Kiislamu na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Miongoni mwa tawfiki za Mwenyezi Mungu kwetu ni kwamba Imam Khamenei (qds), wakati akiwa Rais, alichukua jukumu la kufuatilia masuala ya Hizbullah, na baada ya kukubali uongozi, kwa uangalizi wake wa kipekee alikidhi mahitaji yetu, akajibu maswali yetu ya kisheria na kuiunga mkono jihadi yetu.
Tulijifunza kutoka kwa Bwana wa Mashahidi, Imam Hussein (as), namna ya kuutetea upande wa haki, kuikomboa ardhi, kuishi kwa heshima na utukufu na kuibeba bendera ya Uislamu hata kama kujitolea kungekuwa kugumu.
Leo hii, tangu kuanzishwa kwa Muqawama wa Kiislamu, tunakabiliwa na mapambano makali zaidi dhidi ya jitu la Kizayuni mvamizi; jitu ambalo linaungwa mkono na twaghuti wa Marekani, linalowaua watoto, wanawake na wanaume, kubomoa nyumba na mashamba na kuwafukuza watu kutoka katika ardhi zao.
Limefanya hivyo Ghaza ambapo zaidi ya watu elfu themanini wamepata shahada, na pia Lebanon ambapo tangu tarehe 7 Oktoba 2023 hadi sasa zaidi ya watu elfu kumi wamepata shahada.
Bwana wetu mtukufu, kiongozi wa njia ya Muqawama nchini Lebanon, Sayyid Hassan Nasrallah (ra), pamoja na Sayyid Hashimi, makamanda na mashahidi wengine walipata shahada, lakini sisi tumebaki imara uwanjani kwa msaada wa Unabii wa Muhammad, Wilayah ya Ali, mapenzi ya Maimamu na kumngojea Sahibul-Asr waz-Zaman (aj).
Vijana wa Muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon walikabiliana na zaidi ya wanajeshi na maafisa 90,000 wa jeshi la Israel, pamoja na silaha zao za kisasa za ardhini, baharini na angani; silaha ambazo kila siku huongezewa risasi na vifaa vya kijeshi kupitia ndege za Marekani.


Maoni yako